Idara inayosimamia haram imesema: Tunatumia vifaa maalum kusafisha na kung’arisha dirisha la Maqaam tukufu.

Idara inayosimamia haram katika Atabatu Abbasiyya tukufu imesema kuwa, tunatumia vifaa maalum kusafisha na kung’arisha dirisha la Maqaam ya Imamu Mahadi (a.f).

Kiongozi wa idara ya ufundi Sayyid Haitham Ali amesema “Hakika watumishi wa idara yetu husafisha dirisha la Maqaam ya Imamu wa Zama (a.f) kila wakati kwa kutumia vifaa maalum vya kung’arisha dhahabu na fedha”.

Akaongeza kuwa “Kazi hiyo hufanywa kwa utaratibu maalum, sambamba na kuchagua muda wenye idadi ndogo ya mazuwaru, ili kuepusha usumbufu katika ibada zao na kwa kutumia vifaa maalum kwa umakini mkubwa hasa sehemu zenye (dhahabu na fedha)”.

Idara inayosimamia haram tukufu inamajukumu mengi, miongoni mwa majukumu yake ni kuhudumia mazuwaru, kushindikiza wazee, kurahisisha uingiaji na utokaji ndani ya haram na kusukuma mikokoteni au viti-mwendo vya watu wenye ulemavi au wasioweza kutembea kutokana na maradhi au sababu yeyote.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: