Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, inaendelea na mahafali za (Mimbari za nuru) za usomaji wa Qur’ani katika mkoa wa Diyala.
Kikao cha usomaji wa Qur’ani kimefanywa ndani ya jengo la Husseiniyya ya Abutwalib (a.s) na kuhudhuriwa na watu wengi sana, hafla hiyo imesimamiwa na kituo cha miradi ya Qur’ani chini ya Majmaa.
Wasomaji wa Qur’ani kutoka kwenye Ataba tofauti za Iraq wameshiriki, miongoni mwao ni msomaji wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Ammaar Alhilliy, msomaji wa Atabatu Alawiyya Sayyid Hani Mussawi na msomaji wa Atabatu Kadhimiyya Dokta Raafii Al-Aamiri, muongozaji wa hafla alikuwa ni Sayyid Muhammad Baaqir Aali Sarsuuh.