Kitengo cha usimamizi wa majengo ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya, kinakarabati njia zinazoelekea kwenye malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Kiongozi wa idara ya ujenzi Sayyid Muhammad Abdu-Nabi amesema “Kazi ya ukarabati inafanywa chini ya maelekezo ya uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya kupitia katibu mkuu Sayyid Mustwafa Murtadha Aali Dhiyaau-Dini, kama sehemu ya kuwahudumia mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s)”.
Akasema kuwa kazi ya ukarabati inahusisha njia nyingi zinazoelekea kwenye malalo takatifu sambamba na kukarabati vyoo vinavyo tumiwa na mazuwaru vilivyopo kwenye barabara hizo na katika maeneo yanayozunguka Ataba tukufu.