Wasimamizi wa kongamano ni kitengo cha habari na utamaduni, taasisi ya Alwaafi ya utafiti na uhakiki na jumuiya ya Al-Ameed chini ya kauli mbiu isemayo “Marjaa Dini ni ngao ya umma wa kiislamu” siku ya mwezi (12 Dhulqaadah 1444h) sawa na tarehe (1/6/2023m) ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) na litadumu kwa siku mbili.
Kongamano hilo litakuwa na vipengele vifuatavyo:
- Kikao cha kielimu tafiti kuhusu mfumo wa Marjaa-Dini mkuu na nafasi yake ya kipekee na kibinaadamu.
- Shindano la mashairi.
- Shindano la kisa kifupi.
- Shindano la filamu fupi.
Washindi wa mashindano hayo watatangazwa siku ya pili ya kongamano ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) katika Atabatu Abbasiyya, washindi watapewa zawadi na kutolewa tuzo kwa vyombo vya habari.