Idara ya maelekezo ya kidini imefanya hafla ya kuadhimisha mazazi ya Imamu Ridhwa (a.s).

Idara ya maelekezo ya kidini tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya, imefanya hafla kubwa ndani ya Sardabu ya Imamu Mussa Alkadhim (a.s) katika maadhimisho ya kumbukumbu ya kuzaliwa Imamu Ridhwa (a.s).

Kiongozi wa idara hiyo bibi (Adhraa Shami) amesema: “Hafla imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyofuatiwa na mhadhara wa kidini kutoka kwa kiongozi wa idara ya mahusiano na matukio ya kidini bibi Rajaa Ali ambaye ameongea kuhusu historia tukufu.

Akaendelea kusema “Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya imeshiriki kwa kuimba qaswida za kuonyesha mapenzi kwa Imamu Ridhwa (a.s)”.

Hafla ikahitimishwa kwa kipengele cha maswali na utoaji wa zawadi kwa waliojibu vizuri.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: