Katibu mkuu wa Atabatu Husseiniyya Mhandisi Hassan Rashidi Al-Abaaiji, amesema kuwa fatwa ya kujilinda ilitoa somo kwa maadui wa Iraq na imeonyesha uwezo wa raia wake katika kulinda taifa lao na maeneo matakatifu.
Ameyasema hayo katika kongamano la kuadhimisha kutolewa kwa fatwa tukufu ya kujilinda awamu ya saba, linalosimamiwa na kitengo cha Habari na utamaduni, taasisi ya Alwaafi na jumuiya ya Al-Ameed katika Atabatu Abbasiyya chini ya kauli mbiu isemayo (Marjaa-Dini ni ngome ya umma wa kiislamu). Ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s).”.
Akasema “Leo tunaadhimisha mwaka wa saba tangu ilipotolewa fatwa tukufu ya kujilinda na Marjaa-Dini mkuu katika mji wa Najafu, lau kama sio fatwa hiyo magaidi wangeangamiza taifa la Iraq na kuharibu maeneo matakatifu, hakika fatwa hiyo ndio ilizuwia njama na magaidi”.
Akaogeza kuwa “Fatwa ya kujilinda ilitoa somo kubwa kwa magaidi na maadui wa Iraq, hakika raia wa Iraq wanauwezo wa kulinda taifa lao na maeneo matakatifu pamoja na kulinda umoja wa taiafa na usalama”.
Akatoa shukrani nyingi kwa wote waliojitolea damu na mali zao kwa ajili ya kulinda taifa la Iraq, akasema kuwa walichofanya wapiganaji wa kujitolea na wale wa jeshi tukufu la Iraq kinastahiki pongezi kubwa.