Rais wa kamati ya kuhakiki mauwaji ya Spaikar amesema: Kuzindua kitabu cha mauwaji wa Spaikar ni ushindi wa damu za mashahidi.

Rais wa kamati ya kuhakiki mauwaji ya Spaikar jaji Yaasir Alkhuzai amesema kuwa, kuzindua kitabu cha mauwaji ya Spaikar ni ushindi wa damu za mashahidi.

Alkhuzai ameviambia vyombo vya Habari kuwa “Uzinduzi wa kitabu hiki ni kuelimisha vizazi vijavyo kuhusu ugaidi uliofanywa, nalo ni jambo kubwa kufanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu”. Akasema “Uhakiki uliofanywa umewezesha kukamatwa magaidi wengi walioshiriki kwenye mauwaji hayo”.

Akasema kuwa “Hadi sasa mahakama ya makosa ya jinai imesha toa hukumu za kunyongwa hadi kufa kwa magaidi 116 waliokutwa na hatia ya mauwaji hayo, hukumu nyingi zimethibitishwa na mahakama kuu”.

Akafafanua kuwa “Hadi sasa magaidi waliohukumiwa kunyongwa hadi kifo 37 wamesha nyongwa, nao ni wale wahusika wakuu wa mauwaji hayo, bado juhudi za kuwatafuta na kuwakamata magaidi waliobaki zinaendelea hadi wote waliohusika kwenye mauwaji yale wafikishwe mahakamani”.

Siku ya kwanza ikahitimishwa kwa kuwapa zawadi watafiti walioshiriki kuandika kitabu cha mauwaji ya Spaikar kutoka kwa kiongozi wa idara ya Atabatu Abbasiyya Dokta Abbasi Rashidi Mussawi, sambamba na kutoa zawadi kwa taasisi zilizosaidia uandishi wa kitabu hicho, kutoka ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria Sayyid Afdhalu Shami, rais wa Majmaa-Ilmi katika Atabatu Abbasiyya Dokta Mushtaqu Ali, rais wa kitengo cha mahusiano Sayyid Muhammad Ali Azhar, rais wa kitengo cha Habari na utamaduni Sayyid Aqiil Yaasiri sambamba na kutoa mkono wa pole kwa familia za mashahidi wa Spaikar, miongoni mwa zawadi walizopewa ni vitu vya kutabaruku na Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: