Kuanza kwa shughuli za jioni ya siku ya pili ya kongamano la kuadhimisha fatwa tukufu ya kujilinda.

Shughuli za kongamano la kuadhimisha fatwa tukufu ya kujilinda awamu ya saba zinaendelea katika Atabatu Abbasiyya jioni ya siku ya pili.

Shughuli hiyo imehudhuriwa na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu sambamba na kuhudhuriwa na viongozi wengi wa kidini na kisekula kutoka ndani na nje ya Iraq.

Kongamano hilo limeratibiwa na kitengo cha habari na utamaduni, taasisi ya Alwaafi na jumuiya ya Al-Ameed kwa ajili ya kuadhimisha kumbukumbu ya kutolewa kwa fatwa ya kujilinda, chini ya kauli mbiu isemayo (Marjaa-Dini ni ngome ya umma wa kiislamu) ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s).

Ratiba ya jioni inahusisha ujumbe kutoka kwa kamati ya maandalizi na kutangazwa majina ya washindi wa shindano la mashairi lililofanywa katika kongamano hilo.

Ratiba itahitimishwa kwa kugawa zawadi kwa washindi, wanahabari na baadhi ya watu waliochangia kufanikisha kwa kongamano hili.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: