Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake inaendelea na semina za majira ya kiangazi katika mji wa Karbala.

Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya inaendelea na semina za majira ya kiangazi katika mji wa Karbala.

Maahadi inafanya juhudi ya kufikia malengo yake matukufu katika jamii kwa kufanya semina za wanafunzi wa shule za msingi na sekondari katika masomo ya kuhifadhi Qur’ani tukufu, Fiqhi, Lugha na uchoraji.

Semina hizo zinafanywa katika matawi yote kwa lengo la kuwafundisha mambo yenye manufaa kwao duniani na akhera, sambamba na kutambua uwepo wa vipaji kwa kila mwanaadamu vinavyotakiwa kuibuliwa na kuendelezwa.

Maahadi ya Qur’ani tukufu inaendelea kufanya semina na nadwa mbalimbali kwa lengo la kuitumikia Qur’ani na kueneza utamaduni wa kusoma Qur’ani katika jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: