Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, inafanya semina za Qur’ani za majira ya kiangazi kwa wanafunzi wa Karbala na mikoa mingine.
Semina zinafanywa kwa kushirikiana na Maahadi ya Qur’ani tukufu chini ya Majmaa, katika mkoa wa Karbala, Baabil, Bagdad, Diwaniyya, Najafu, Muthanna, Waasit, Dhiqaar, Kirkuuk na Diyala.
Wanufaika wa semina hizo wanafika elfu 54 kutoka mikoa 10 ikiwa ni sehemu ya kunufaika na likizo za majira ya kiangazi.
Semina zinalenga mabinti wenye umri wa miaka saba hadi 17, wanapewa malezi bora kwa misingi ya Qur’ani tukufu.
Maahadi ya Qur’ani chini ya Majmaa, inatoa huduma nyingi kwa wanafunzi wanaoshiriki kwenye semina hizo, miongoni mwa huduma ni usafiri wa bure kutoka majumbani kwaho hadi sehemu wanazo somea na kurudi, kugawa vitabu vya masomo na ratiba ya vipindi vya mapumziko.