Semina kama hizo zinafanywa katika mikoa ya Karbala, Baabil, Bagdad, Diwaniyya, Najafu, Muthanna, Waasit, Dhiqaar, Kirkuuk na Diyala.
Wanafundishwa kuhifadhi Qur’ani, Fiqhi, Aqida, Akhlaq, Historia ya Ahlulbait (a.s) pamoja na masomo ya ufundi na michezo, yote kwa ujumla yanalenga kujenga utamaduni wa kufuata mwenendo wa vizito viwili.
Wanufaika wa mradi wa semina hizo ni zaidi ya elfu 54 kutoka mikoa 10 ya Iraq, zinalenga mabinti wenye umri wa mika saba hadi 17. Wanafundishwa malezi bora kwa kufuata misingi ya Qur’ani tukufu.
Maahadi ya Qur’ani chini ya Majmaa, inatoa huduma nyingi kwa wanafunzi wanaoshiriki kwenye semina hizo, miongoni mwa huduma ni usafiri wa bure kutoka majumbani kwaho hadi sehemu wanazo somea na kurudi, kugawa vitabu vya masomo na ratiba ya vipindi vya mapumziko.