Majmaa-Ilmi imegawa vitabu vya kufundishia elfu 54 kwa wanafunzi wanaoshiriki kwenye semina za Qur’ani za majira ya kiangazi.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imegawa vitabu vya kufundishia elfu 54 kwa wanafunzi wanaoshiriki kwenye semina za majira ya kiangazi.

Majmaa imegawa vitabu hivyo kwa wanafunzi wote katika siku ya kwanza ya semina, vitabu hivyo vimechapishwa na Daarul-Kafeel chini ya Atabatu Abbasiyya kwa ubora mkubwa.

Vitabu vya kufundishia vimeandikwa na Atabatu Abbasiyya rasmi kwa ajili hiyo, vinamasomo ya Qur’ani, Aqida, Fiqhi, Akhlaq, na Sira, vina picha, michoro na maandishi mazuri yanayosomeka kwa urahisi.

Semina zinafanywa kwenye mikoa tofauti, kama vile: Karbala, Najafu, Baabil, Bagdad, Diwaniyya, Muthanna, Waasit, Dhiqaar, Kirkuuk na Diyala, zaidi ya wanafunzi 54,000 wanashiriki kwenye semina hizo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: