Majmaa-Ilmi imezindua mradi wa semina za Qur’ani katika majira ya kiangazi kwenye mkoa wa Muthanna.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imezindua mradi wa semina za Qur’ani katika majira ya kiangazi kwenye mkoa wa Muthanna, ambapo jumla ya semina (50) zitafanywa kwenye wilaya na vitongoji vya mkoa huo.

Semina hizo zinasimamiwa na Maahadi ya Qur’ani tukufu chini ya Majmaa.

Hadi sasa tumeshapokea zaidi ya wanafunzi (2000) watakao fundishwa masomo ya Aqida, Akhlaq na usomaji wa Qur’ani, aidha tunawalimu zaidi ya (80).

Maahadi inatoa huduma nyingi za bure kwa wanafunzi, miongoni mwa huduma hizo ni usafiri wa kwenda na kurudi darasani, chakula na vitabu vya masomo wanayofundishwa.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu inalenga kutumia vizuri wakati wa likizo za kiangazi kwa kuinua kiwango cha elimu ya Dini kwa wanafunzi hao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: