Mmoja wa wahitimu wa digrii ya pili (Masta) ameandika kuhusu malikale zilizopo kwenye makumbusho ya Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu.
Mtafiti bwana Wasaam Abdulhamidi amesema kuwa “Andiko limejikita katika kueleza siraha zilizopo ndani ya makumbusho ya Alkafeel kuanzia mwaka (1533m sawa na 939h hadi 1918m sawa na 1336h), andiko hilo limetaja umbo, aina, mapambo, nakshi, utengenezwaji wake na kama siraha hiyo ni ya kujilinda au kushambulia”.
Akaongeza kuwa “Andiko limeeleza taarifa za kitafiti kuhusu aina za saraha zilizokuwa zinatumika wakati wa utawala wa Othumaniyya katika makumbusho ya Alkafeel nchini Iraq”.
Akaendelea kusema “Makumbusho ya Alkafeel imetunza siraha adimu za kujilinda na kushambulia zilizotumika wakati wa utawala wa Othumaniyya pamoja na maelezo ya kina kwa kila siraha”.