Kitengo cha maarifa kimetoa jarida la (22) la Radu-Shamsi.

Hivi karibuni kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya, kimetoa jarida la (22) la Radu-Shamsi linaloandika kuhusu turathi za mji wa Hilla.

Wasimamizi wa uchapishaji wa jarida hilo ni kituo cha turathi za Hilla.

Toleo hili limeandika maudhui zinazohusu mji wa Hilla kihistoria, ikiwa ni pamoja na kuelezea familia za watu wa Hilla, familia ya “Aalul-Idhaari” imechukua nafasi kubwa katika mlango huo.

Matukio ya kitamaduni pia yamepewa nafasi kubwa, bila kusahau kuelezea watafiti na waandishi wa mkoa huo, kunamlango maalum unaeleza mashahidi wa fatwa tukufu ya kujilinda na mengineyo mengi.

Hili ni miongoni mwa majarida muhimu katika mji wa Hilla, linaandika mambo tofauti yanayohusu mji wa huo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: