Kitengo cha uboreshaji kinashiriki kwenye nadwa inayohusu ukosefu wa ajira.

Kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu katika Atabatu Abbasiyya, kimeshiriki kwenye nadwa iliyofanywa na kituo cha mito miwili cha tafiti za kimkakati na kuhudhuriwa na taasisi tofauti.

Kitengo kimeeleza visa vya mafanikio ya miradi inayofanywa na Atabatu Abbasiyya na namna ya kunufaika na miradi hiyo katika utoaji wa ajira.

Kitengo kimejata nafasi ya miradi ya Atabatu Abbasiyya kwenye sekta ya afya, viwanda na kilimo katika utoaji wa ajira.

Washiri wa nadwa hiyo wamepongeza kazi kubwa inayofanywa na Ataba ya kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira, wakaitakia mafanikio zaidi katika miradi yake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: