Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya imepokea wanafunzi (225) kupitia program ya mapumziko.
Wanafunzi hao wanaumri wa miaka (8 – 10) kutoka shule ya awali ya Najafu ambayo ipo chini ya Maahadi.
Kiongozi wa Maahadi bibi Manaar Aljaburi amesema “Program ya mapumziko inahusisha wanafunzi wa semina za majira ya kiangazi wa shule za msingi, ziara kama hizi vinalenga kutia furaha katika nafsi zao sambamba na kunufaika na mafundisho ya Dini”.
Akaongeza kuwa “Program inamambo mengi muhimu yanayo saidia kuwajenga wanafunzi kimaadili, miongoni mwa mambo hayo ni: Adabu za kuingia katika nyumba, Ubora wa kushauriana, Dhana nzuri kwa wengine, Umuhimu wa mwanafunzi kutambua wajibu wake na mambo muhimu yanayohusu mabinti”.