Kituo cha utamaduni wa familia katika Atabatu Abbasiyya kinafanya semina ya kuwajengea uwezo wanahabari kwa kutumia program ya (Adobe Premiere).
Mkufunzi wa semina hiyo ni bwana Ali Rasuul kutoka kituo cha utengenezaji wa vipindi chini ya kitengo cha habari.
Semina hiyo inawahusisha watumishi wa kituo na idara ya wanawake chini ya Ataba, kwa lengo la kuboresha utendaji wao na uandaaji wa vipidhi vinavyojikita katika kujenga familia kwa kufuata mwenendo wa Ahlulbait (a.s).
Kituo kinautaratibu wa kuwajengea uwezo watumishi wake, ili waweze kujenga familia bora katika jamii na kuleta utulivu wa mafsi na familia.