Shule za Al-Ameed chini ya kitengo cha malezi na elimu, zimefanya kikao kikubwa cha walimu wa kuu wa shule za wavulana.
Kikao hicho kimeitishwa na mkuu wa shule hizo Dokta Haidari Al-Aaraji.
Kikao kinahusu kupongezana kutokana na ufaulu mzuri waliopata kwenye mitihani ya darasa la sita mwaka huu, na kuwahimiza kuongeza juhudi na kulinda mafanikio hayo, bali mafanikio ya mwakani yawe makubwa zaidi ya hayo.
Kikao kimepambwa na majadiliano ya namna ya kutoa mafunzo msasa kwa viongozi wa idara na walimu wakati wa likizo za majira ya kiangazi, ili kuwaandaa na msimu mpya wa masomo sambamba na kuandaa mahitaji yoto yatakayofanikisha kazi yao.
Washiriki wameongea kuhusu umuhimu wa kuandaa na kugawa kwa ufanisi baadhi ya majukumu ya kiidara na baadhi ya vitendea kazi muhimu kama vitabu vya masomo na sale maalum kwa shule za Al-Ameed.
Wakahitimisha kikao kwa kujadili mambo ya kiidara kwa kila shule.