Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, inafanya shughuli mbalimbali katika ratiba ya semina za majira ya kiangazi kwenye mtaa wa Hamza magharibi ya mji wa Baabil.
Semina hizo zinasimamiwa na Maahadi ya Qur’ani tukufu chini ya Majmaa.
Kiongozi wa Maahadi katika mji wa Baabil Sayyid Muntadhwiri Mashaikhi amesema “Vikao vya usomaji wa Qur’ani vinahusisha uimbaji wa qaswida na mashairi ya kusifu kizazi kitakasifu”.
Akaongeza kuwa “Kuna program nyingi zinazofanywa katika mradi huu, kuna vikao vya usomaji wa Qur’ani, mashindano na program maalum ya utambuzi wa vipaji vya wanafunzi kwa lengo la kuviendeleza na kuwaingiza kwenye program nyingine ya wenye vipaji”.