Hospitali ya Alkafeel imefanikiwa kuondoa tatizo la kuzaliwa nalo kwa mtoto mwenye umri wa miaka miwili.

Jopo la madaktari katika hospitali ya Alkafeel, limefanya upasuaji wa kuondoa tatizo la kuzaliwa nalo kwa mtoto wa miaka miwili.

Daktari bingwa wa urekebishaji wa aibu za kimaumbile katika hospitali ya Alkafeel Dokta Husam Al-Ambaari amesema: “Mtoto mwenye umri wa miaka miwili alikuwa na tatizo la ukuaji wa baadhi ya viungo vyake, baada ya kufanyiwa vipimo akagundulika kuwa na tatizo la kimaumbile kwenye uti wa mgongo”.

Akaongeza kuwa “Tumemfanyia upasuaji kwa kuondoa tatizo lililokuwepo kwenye uti wa mgongo”.

Akasisitiza kuwa “Upasuaji umefanyika kwa mafanikio na mgongwa ameruhusiwa kurudi nyumbani akiwa na afya nzuri”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: