Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya inaendelea kufundisha Qur’ani wanafunzi wa semina za majira ya kiangazi katika mji mkuu wa Bagdad.
Wanafunzi zaidi ya elfu tisa (9000) wanashiriki kwenye semina hizo, miongoni mwa masomo yanayofundishwa ni Fiqhi, Aqida, Sira na Akhlaq, masomo yote yamepangiwa mfumo maalum unaoendana na umri wa washiriki.
Mradi wa semina za Qur’ani upo katika wilaya zote za mji mkuu wa Bagdad hadi kwenye vitongoji na mitaa.
Majmaa-Ilmi inalenga kutumia vizuri wakati wa likizo za kiangazi kwa kufundisha Qur’ani tukufu na maarifa ya Dini.