Kila siku.. ofisi inayosimamia haram tukufu inaendelea na kazi ya kusafisha mapambo ya haram.

Idara ya mafundi chini ya ofisi inayosimamia haram ya Atabatu Abbasiyya inaendelea na kazi ya kusafisha mapambo ya haram kila siku.

Kiongozi wa Idara Sayyid Haitham Ali amesema “Tunasafisha vumbi kwenye mapambo na kung’arisha kwa kutumia vifaa maalum, ikiwa ni pamoja na winchi ili kuweza kufikia kwa urahisi mapambo yote yaliyopo ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Akafafanua kuwa: “Kazi hiyo tunaifanya nyakati ambazo huwa na mazuwaru wachache, ili kuepusha usumbufu”. Akasema kuwa “Kazi hii tunafanya kila siku ndani ya mwaka mzima kwa lengo la kulinda ubora wa mapambo ya haram na uzuri wake”.

Ofisi inayosimamia haram tukufu inamajukumu mengi, miongoni mwa majukumu yake ni kufanya usafi na kuongoza matembezi ya mazuwaru wanaoingia na kutoka ndani ya malalo takatifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: