Kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya kimeboresha mbinu za utunzaji wa mali za mazuwaru.
Idara inayohusika na kutunza mali za mazuwaru (Amanaat) imeandaa maeneo nane ya kutunza mabeji ya mazuwaru, kwa ajili ya kuwafanyia wepezi katika kufanya ibada.
Makamo rais wa kitengo cha utumishi Sayyid Abbasi Ali amesema “Kazi ya idara yetu ni kutunza mali za mazuwaru (vifaa na mabeji), tunafanya hivyo kwa umakini mkuwa wakati wa kupokea na kutoa”.
Akaongeza kuwa “Tumeandaa sehemu nane zinafanya kazi muda wote, zipo upande wa mlango wa Qibla, mlango wa Alqami, mlango wa Imamu Hassan na mlango wa Imamu Alkadhim (a.s), kwa lengo la kuhudumia mazuwaru na kurahisisha utendaji wao wa ziara”.
Akaendelea kusema “Kazi za watumishi wa kitengo huongezeka siku za ziara ya Arubainiyya na ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu, kutokana na kuwepo kwa watu wengi wanaokuja kumzuru Abulfadhil Abbasi (a.s)”.
Atabatu Abbasiyya huratibu kwa umakini mkubwa ziara na kuwafanya mazuwaru wafanye ibada zao kwa amani na utulivu.