Kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu katika Atabatu Abbasiyya, kinafanya ukarabati wa gari za kutumia umeme ambazo husaidia kubeba mazuwaru.
Ukarabati huo unasimamiwa na idara ya mafundi chini ya ofisi ya kubeba mazuwaru.
Kiongozi wa idara Sayyid Hasanaini Ali amesema “Kitengo hufanya ukarabati wa gari zinazotumia umeme ambazo ni maalum kwa ajili ya kubeba mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi kila wakati”.
Akaongeza kuwa “Idara ya ukarabati hutengeneza gari zote zinazo haribika sambamba na kufanya ukaguzi wa mara kwa mara, ikiwa ni pamoja na kufanya matengenezo ya viti-mwendo vya umeme na winchi”.
Akafafanua kuwa “Kazi ya kukagua na kufuatilia utendaji wa gari na mitambo hiyo inafanywa kila siku na watumishi wa idara hii, hakika Atabatu Abbasiyya inahakikisha vitengo vyake vyote vinatoa huduma bora kwa mazuwaru”.