Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya inafanya nadwa za Qur’ani kwa wanafuni wa sekondari (upili).
Mmoja wa wakufunzi Ustadhat Zahara Hassan amesema: “Idadi ya washiriki imefika (900), wanafundishwa Fiqhi, Aqida, Akhlaq na hukumu za tajwidi, aidha wanafundishwa masomo ya ufundi na michezo kulingana na umri wao”.
Akaongeza kuwa “Nadwa zimepata muitikio mkubwa kutokana na masomo yanayofundishwa kuwa na faida katika dini yao na maisha” akabainisha kuwa “Wanasoma siku tano kwa wiki”.
Idara ya wahadhiri ya Husseiniyya tawi la wanawake inalenga kunufaika na kipindi hiki cha likizo za wanafunzi kwa kufundisha Qur’ani tukufu.