Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini amegagua miradi ya Ataba tukufu.
Mheshimiwa katibu mkuu amefatana na mkuu wa ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Dokta Afdhalu Shami.
Mheshimiwa katibu mkuu ameangalia huduma zinazotolewa na Atabatu Abbasiyya kwa mazuwaru na wakazi wa Karbala kwa ujumla.
Katibu mkuu amesema kuwa Atabatu Abbasiyya inatoa kipaombele zaidi katika kuimarisha usalama wa mazuwaru na kuhakikisha taasisi za kutoa huduma zinafanya kazi katika mazingira salama.
Ziara hii ni sehemu ya ratiba maalum ya katibu mkuu ya kutembelea miradi na huduma zinazotolewa na Atabatu Abbasiyya kwa mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).