Vijiji vingi vya mkoa wa Dhiqaar vimeshuhudia semina za Qur’ani zinazosimamiwa na Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya.
Mradi huo unaendeswa na Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Dhiqaar chini ya Majmaa, ukiwa na washiriki zaidi ya wanafunzi 2250 na walimu 80 kwenye zaidi ya misikiti 70.
Misikiti na Husseiniyya za mji wa Naswiriyya zimepata mahudhurio makubwa ya wanafunzi wa semina za Qur’ani mwaka huu, kuna walimu mahiri wanaofundisha Qur’ani tukufu, Aqida, Fiqhi, Akhlaq na Sira.
Wananchi wameshukuru Atabatu Abbasiyya kwa kuendesha mradi huu.
Wanafunzi zaidi ya 54000 wananufaika na mradi huu kutoka mikoa (12) ya Iraq, wanafundishwa Qur’ani, Aqida, Fiqhi, Akhlaq na Sira.