Majmaa-Ilmi yafanya harakati za mazowezi na ufundi kwa wanafunzi wa semina za Qur’ani.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imeandaa ratiba ya michezo na ufundi kwa wanafunzi wa semina za Qur’ani katika mji wa Karbala.

Mkuu wa Maahadi ya Qur’ani tukufu shekhe Jawadi Nasrawi amesema “Ratiba ya mradi inalenga kunufaika na kipindi cha likizo ya majira ya kiangazi kwa kufundisha mambo mbalimbali”.

Akaongeza kuwa “Wanafunzi wamevutiwa sana na ratiba hiyo sambamba na kupata faida kubwa katika masomo ya Qur’ani”.

Majmaa-Ilmi inalenga kunufaika na kipindi cha likizo za wanafunzi kwa kufundisha Qur’ani tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: