Mgeni mmoja ambaye ni mhadhiri wa chuo, amesema: “Nimetembelea makumbusho ya Alkafeel katika Atabatu Abbasiyya nikiwa na wenzangu (14) kutoka Hispania, tumeangalia malikale zilizopo kwenye makumbusho hiyo”.
Akaongeza kuwa “Tumevutiwa sana na mpangilio mzuri wa malikale hizo, akasema kuwa ziara ilikuwa nzuri na yapekee”.
Akaendelea kusema “Tumetembelea sehemu nyingi za kihistoria nchini Iraq, ikiwa ni pamoja na makumbusho ya Baabil, hakika mambo mazuri tuliyoyaona tutaenda kuwahadithia jamaa zetu wa Hispania na tutawahimiza waje kutembea Iraq”.