Wageni kutoka nchini Hispania: Shule za Al-Ameed ni mfano mwema wa malezi.

Wageni kutoka nchini Hispania wamesema kuwa shule za Al-Ameed chini ya Atabatu Abbasiyya ni mfano mzuri wa malezi.

Yamesemwa hayo wakati wajumbe wa taasisi ya Ahlulbait kutoka Hispania walipotembelea shule za Al-Ameed.

Mmoja wa wageni hao Dokta wa tafiti za kiarabu na kiislamu Yusufu Harnandizi amesema “Wakati wa ziara yetu katika shule za Al-Ameed tumeona kuwa zinamiliki vifaa vya kisasa zaidi, hakika shule hizi ni mfano bora wa malezi”.

Akaongeza kuwa “Tumeona kuwa shule za Al-Ameed zinavifaa vyote vya kisasa vya kufundishia pamoja na viwanja vizuri vya michezo na sehemu za kupumzika wanafunzi”.

Akasisitiza kuwa “Taasisi ya elimu katika Atabatu Abbasiyya inafamafanikio makubwa na wanafunzi wanaufaulu mzuri”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: