Majmaa-Ilmi imefika hatua ya mwisho katika maandalizi ya mradi wa kiongozi wa wasomaji kitaifa.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imefika katika hatua ya mwisho ya maandalizi ya mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa.

Harakati hiyo inasimamiwa na kituo cha miradi ya Qur’ani chini ya Majmaa.

Mkuu wa kituo Sayyid Hasanaini Halo amesema “Watumishi wa kituo cha miradi ya Qur’ani wanaendelea na maandalizi ya awamu mpya ya mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa”.

Akaongeza kuwa “Tupo katika hatua za mwisho katika maandalizi ya mradi”, akasema “Tunatarajia kuanza kupokea wanafunzi watakaoshiriki kwenye mradi huu siku chache zijazo”.

Kituo cha miradi ya Qur’ani ni moja ya sehemu za Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu, kinalenga kueneza elimu ya Qur’ani katika jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: