Rais wa Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya Dokta Mushtaqu Ali, amekagua maandalizi ya mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa.
Maandalizi hayo yanafanywa na kituo cha miradi ya Qur’ani chini ya Majmaa.
Amekagua kumbi za madarasa na mambo mengine yanayofungamana na mradi huo, kama vile misikiti, viwanja vya michezo na sehemu za kutolea huduma mbalimbali.
Amehimiza kuwepo kwa ushirikiano baina ya kituo cha miradi ya Qur’ani na vitengo vya Ataba tukufu katika kutatua changamoto zote na kupanga siku rasmi ya kuanza masomo.
Kituo cha miradi ya Qur’ani ni moja ya sehemu za Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu, kinalenga kueneza elimu ya Qur’ani katika jamii.