Katika mji wa Kirkuuk.. Ugeni wa Majmaa-Ilmi umetembelea semina za Qur’ani.

Ugeni kutoka Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, unatembelea mradi wa semina za Qur’ani katika majira ya kiangazi mkoani Kirkuuk.

Msaidizi wa kitengo cha malezi amemuambia rais wa Majmaa-Ilmi na rais wa ugeni huo Dokta Ibrahim Mirza kuwa “Hakika ziara hii ni sehemu ya kuangalia maendeleo ya semina za Qur’ani zinazoendelea wakati huu wa kiangazi, kwa lengo la kuangalia maendeleo yake kwa ujumla, aidha kuangalia kama kuna mahitaji yeyote kwa wanafunzi na walimu sambamba na kusikiliza maoni yao ya namna ya kuboresha semina hizi ili tuweze kufikia malengo yaliyokusudiwa”.

Akaongeza kuwa “Tumeona uwajibikaji mkubwa wa walimu na wanafunzi wa semina hizi” akasema: “Ugeni umekuja na bendera za Abulfadhil Abbasi (a.s) na kuzitoa zawadi kwa wawakilishi wa Maraajii na viongozi walio saidia kufanyika semina hizi”.

Akabainisha kuwa “Semina za Qur’ani zinazofanywa na Majmaa-Ilmi katika mkoa wa Kirkuuk, zinahudhuriwa na wanafunzi zaidi ya (2000) kutoka kwenye misikiti na Husseiniyya (63) na walimu wapo (18)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: