Katika mji wa Baabil.. Majmaa-Ilmi inafanya nadwa pamoja na wazazi wa wanafunzi wanaoshiriki kwenye semina za majira ya kiangazi.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imefanya nadwa pamoja na wazazi wa wanafunzi wanaoshiriki kwenye semina za Qur’ani katika majira ya kiangazi mkoani Baabil.

Mhadhiri wa nadwa hiyo alikuwa ni Dokta Haidari Shalaa chini ya anuani isemayo (Kunufaika na likizo katika kuendeleza vipaji vya wanafunzi kutokana na juhudi za Majmaa-Ilmi na wazazi), wasimamizi wa nadwa hiyo ni Maahadi ya Qur’ani tawi la Baabil chini ya Majmaa.

Nadwa inalenga kuwa na misingi ya pamoja katika kutengeneza kizazi kinacho fungamana na mafundisho ya Qur’ani tukufu.

Watumishi wa Majmaa kupitia Maahadi ya Qur’ani tawi la Baabil, wanafanya kila wawezalo katika kutumikia kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi kitakatifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: