Kuna zaidi ya wanafunzi elfu moja wanaosoma kwenye semina za Qur’ani zinazosimamiwa na Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika wilaya ya Mashkhabu mkoani Najafu.
Semina hizo zinasimamiwa na Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Najafu chini ya Majmaa.
Semina za Najafu zipo katika misikiti (14) na kuna walimu (26).
Maahadi hutuma wataalamu kwenye semina hizo kila siku, kwa lengo la kuangalia maendeleo na kubaini mambo yanayo hitajika ili kufikia malengo.