Kitengo cha uboreshaji kinaendelea na warsha ya kuwanoa watumishi wa Atabatu Abbasiyya.

Kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu katika Atabatu Abbasiyya, kinaendelea na warsha ya kuwanoa watumishi wa Ataba tukufu.

Mmoja wa wawezeshaji wa warsha hiyo Sayyid Karaar Maamuri amesema “Warsha ya leo imejikita katika misingi ya utoaji wa huduma, ambayo inaanzia na kutambua, kufahamu, kuchambua, kutekeleza na tathmini”.

Akaongeza kuwa “Warsha inalenga kuandaa washiriki kielimu na kutumia uzowefu wao kama wakufunzi katika Ataba, sambamba na kuwaandaa waweze kuendesha mafunzo yajayo kutokana na kuimarika kwao kielimu na kimaadili”.

Sehemu ya mwisho ya warsha hii itadumu kwa muda wa siku kumi, kwa ajili ya kuwafundisha mambo mengi yanayohitajika katika semina na kubaini ukamilifu na upungufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: