Kitengo cha uhandisi kimeingiza sokoni bidhaa za ujenzi.

Kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya kimeingiza sokoni bidhaa ya ujenzi.

Mkuu wa kituo cha viwanda na ujenzi chini ya kitengo, Mhandisi Basaam Hashimi amesema: “Tumeingiza sokoni mtambo wa uzalishaji unaotumika katika miradi ya ujenzi pamoja na kwenye miradi ya Ataba tukufu”.

Akaongeza kuwa “Mtambo wa kutengeneza tofafi za block kubwa na ndogo ni miongoni mwa mitambo muhimu, unauwezo wa kutengeneza tofali zaidi ya elfu kumi na tisa (19000) kwa siku, asubuhi na jioni, ni mtambo wa kisasa unaotoa tofali zenye ubora mkubwa”.

Naye Mhandisi Mustwafa Qassim mmoja wa watumishi wa kituo hicho amesema: “Mtambo ni mzuri kushinda mitambo mingine, tofali zake zimeonyesha uimara mkubwa sana kwenye vipimo, tofauti na tofali zinazotengenezwa kwenye viwanda vingine vya kisasa, pia unaweza kufanya kazi katika mazingira tofauti”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: