Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wasichana imeanza kufanya mitihani ya mwisho kwa wanafunzi wa semina za Qur’ani.

Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wasichana katika Atabatu Abbasiyya, imeanza mitihani ya mwisho kwa wanafunzi wa semina za Qur’ani katika kituo cha Najafu.

Kiongozi wa Maahadi bibi Manaar Aljaburi amesema kuwa “Mitihani ya mwisho inafanywa kwa mujibu wa ratiba maalum na katika masomo yaliyoteuliwa toka mwanzo, kama vile Nahau, Historia ya Qur’ani na visa vya Qur’ani, semina hii inawashiriki (50)”.

Akaongeza kuwa “Masomo tofauti yamefundishwa, kama vile Hukumu za usomaji, Maarifa ya Qur’ani, misingi ya tafsiri, Nahau, Mantiki, Fiqhi, Aqida na Maarifa ya hadithi, baadae watapewa mitihani ya masomo yote”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: