Kundi la wanafunzi wa Dini wanashiriki kufundisha kwenye mradi wa Qur’ani unaosimamiwa na Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya.
Majmaa-Ilmi imetumia baadhi ya wanafunzi wa Dini katika kufundisha kwenye semina za Qur’ani za majira ya kiangazi, ambapo wanafunzisha Qur’ani, Aqida, Fiqhi, Akhlaq na Sira ya Ahlulbait (a.s).
Wamesambazwa kwenye mikoa yote inayo endesha semina hizo, kumbuka Majmaa-Ilmi inaendesha semina za Qur’ani kwenye mikoa (12) wanufaika wa semina hizo wanakadiriwa kuwa elfu (54), kwa lengo la kuhakikisha wanatumia vizuri kipindi cha likizo kwa kufundisha Qur’ani tukufu.