Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya, kimepokea jopo la washiriki wa uandishi wa kitabu cha mashahidi wa fatwa ya jihadi kifaya ya kujilinda.
Wageni hao ni wataalamu wa mambo mbalimbali kutoka kituo cha turathi za Basra chini ya kitengo.
Mkuu wa kituo Shekhe Mudrik Hasuun amesema “Tumepata mchango mkubwa kutoka kwa mtu mmoja mmoja na kituo, wakati wa kuandika taarifa za mashahidi wa fatwa ya jihadi kifaya ya kujilinda, sambamba na kuandika kitabu cha (Mashahidi wa Aqida na taifa) juzuu la saba, litakalo kamilika hivi karibuni”.
Hasuun akawashukuru wote waliochangia katika uandishi wa taarifa za mashahidi wa fatwa ya jihadi kifaya ya kujilinda, akasema kuwa kazi hiyo inastahiki pongezi.