Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imekamilisha maandalizi ya mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa katika awamu mpya.
Mradi huo unasimamiwa na kituo cha miradi ya Qur’ani chini ya Majmaa.
Rais wa Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu Dokta Mushtaqu Ali, amemteua msomaji wa Ataba Muhammad Ridhwa Zubaidi kuwa mkuu wa kamati ya utendaji ya mradi.
Akasisitiza umuhimu wa masomo ya Qur’ani chini ya misingi ya elimu ya sheria na turathi za Ahlulbait (a.s).
Naye mkuu wa kamati ya utendaji bwana Muhammad Ridhwa Zubaidi amethibitisha kukamilika kwa maandalizi yote, ikiwa ni Pamoja na mkakati wa kulea vipaji vya wanafunzi pembezoni mwa masomo ya Qur’ani.