Mpiga picha wa kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Saamir Husseini ameshinda nafasi ya kwanza kwenye mashindano ya kimataifa yaliyofanyika Urusi yakiwa na washindani zaidi ya laki moja.
Husseini amesema, Shindano lilikuwa na sehemu mbili ambazo ni: picha za kawaida na picha nyeusi na nyeupe, picha zote jumla zilikuwa (445000) zikafaulu kuingia kwenye shindano picha (104814) kutoka nchi (174) na picha ya mtumishi wa Abbasi (a.s) ikashinda nafasi ya kwanza.
Sehemu ya pili zikashindanishwa picha nyeusi na nyeupe (3216), hapo akapata nafasi ya pili katika picha bora (100) kutoka kote duniani.
Akasisitiza kuwa, Ushindi wake kwenye shindano hilo ni ushindi wa taifa la Iraq, hususan mji wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) mji mtukufu wa Karbala.