Mheshimiwa Sayyid Swafi amepokea ugeni kutoka Atabatu Radhawiyya tukufu.

Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi amepokea ugeni kutoka Atabatu Radhawiyya ukiongozwa na kiongozi wao wa kisheria Shekhe Ahmadi Marwi.

Ziara hii imetokana na mualiko wa uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Radhawiyya tukufu.

Mheshimiwa Sayyid Swafi amepokea wageni hao na kuwaambia kuwa, wahudumu wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wanafanya kazi usiku na mchana ya kuhudumia mazuwaru wanaokuja kutoka kila sehemu ya dunia.

Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini na viongozi wa kamati kuu ya Ataba tukufu, Sayyid Liith Mussawi, Dokda Abbasi Didah Mussawi, Sayyid Jawadi Hasanawi na mkuu wa ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria Dokta Afdhalu Shami wamehudhuria kikao hicho.

Wageni wameonyesha furaha kubwa, kukutana na Mheshimiwa Sayyid Swafi, wakashukuru mapokezi mazuri waliyopewa katika Atabatu Abbasiyya, wakafikisha salamu za wahudumu wa Imamu Ridhwa (a.s) kwa kiongozi mkuu wa kisheria na wahudumu wote wa Abulfadhil Abbasi (a.s).

Shekhe Marwi akataja uhusiano wa kihistoria uliopo baina ya Ataba mbili tukufu na ushirikiano wa wanafunzi wa Dini wanaotoka Iraq Kwenda Iran kusoma na kinyume chake.

Mwisho wa kikao hicho wakapeana zawadi za kutabaruku na malalo mbili takatifu, huku wakiambiana maneno mazuri na kuombeana dua ya kuendelea kuwatumikia mazuwaru wa malalo mbili takatifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: