Mradi huo unasimamiwa na kituo cha miradi ya Qur’ani chini ya Majmaa.
Mkuu wa kamati ya utendaji Sayyid Muhammad Ridhwa Zubaidi amesema “Mradi unalenga kuibua vipaji vya usomaji wa Qur’ani kwa vijana wenye umri wa miaka (18) kushuka chini, awamu hii inawashiriki zaidi ya (100).
Akaongeza kuwa “Hatua za mradi zinaanzia ngazi ya awali, huchaguliwa wanafunzi wanaojitambua kisha huendelea ngazi ya kwanza, pili na tatu, hufundishwa mahadhi ya kiiraq na kimisri”.
Akaendelea kusema “Maombi ya kushiriki kwenye mradi huu hutumwa kwa njia ya mtandao, kuna kamati maalum inawajibu wa kupokea maombi na kuwakubali wale waliotimiza masharti”, akabainisha kuwa “Upekee wa awamu hii ni kuwepo kwa masomo ya mahadhi za kimisri katika ngazi ya tatu”.