Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu kinaendelea na ratiba ya (misafara ya kitablghi) kwenye nchi kadhaa za Afrika.
Ratiba hiyo inasimamiwa na Markazi Dirasaati Afriqiyya, ambapo masomo tofauti hufundishwa kama vile Fiqhi, Aqida, kuhuisha matukio ya kidini kwa kufanya majlisi na kutoa mawaidha elekezi, hivi karibuni ratiba hiyo imetekelezwa katika nchi ya Naijeria.
Mkuu wa Markazi Dirasaati Afriqiyya Shekhe Saadi Sataari Shimri amesema “Misafara ya kitablighi katika nchi ya Naijeria inafanywa chini ya usimamizi wa Mubalighi wa Markazi Muhammad Abdullahi Twaibu, imejikita katika kusambaza fikra na elimu ya Ahlulbait (a.s) kwenye miji tofauti, katika misafara hiyo hukutana na wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s)”.
Akasisitiza kuwa ratiba hiyo ni endelevu, akasema: “Twaibu amefanya muhadhara kwa tabaka la vijana wenye anuani isemayo (Nafasi ya elimu katika maisha ya mwanaadamu), amesisitiza umuhimu wa elimu katika mtazamo wa Ahlulbait (a.s) na riwaya zinazohimiza kutafuta elimu”.