Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Muhammad Aljawaadi (a.s) kwa wanafunzi wa semina za Qur’ani katika mtaa wa Huriyyah ndani ya mji wa Najafu.
Majlisi imesimamiwa na Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu chini ya Majmaa.
Semina za Qur’ani tukufu zinazofanywa na Majmaa-Ilmi kwenye mtaa wa Huriyyah katika mji wa Najafu zinawashiriki (1250), pamoja na masomo ya Qur’ani wanafundishwa pia Fiqhi, Aqida na Sira.
Kumbuka kuwa makumi ya majlisi hufanywa na Majmaa-Ilmi kwa wanafunzi wa mradi wa Qur’ani, kwenye mikoa tofauti inayofanya semina hizo, kama sehemu ya kuhuisha utajo wa Ahlulbait (a.s).