Wahudumu wa Ataba mbili tukufu wanaomboleza kifo cha Imamu Jawaadi (a.s).

Wahudumu wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya wanaomboleza kifo cha Imamu Muhammad Aljawaadi (a.s) kupitia maukibu ya kuomboleza.

Maukibu imeanzia ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ikapita kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili na Kwenda hadi kwenye haram ya Imamu Hussein (a.s), maikubu hiyo imeundwa na wahudumu wa Ataba mbili tukufu pamoja na mazuwaru waliokuja katika mji wa Karbala kumpa pole Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa msiba huu.

Baada ya maukibu kuwasili katika haram ya Imamu Hussein (a.s) imefanya majlisi ya kuomboleza, ambapo zimesomwa qaswida na tenzi za majonzi, zilizotaja historia ya Imamu Muhammad Aljawaad (a.s) na dhulma alizofanyiwa.

Wahudumu wa Ataba mbili tukufu katika mji wa Karbala, hufanya maombolezo maalum kwenye kila tukio la kukumbuka kifo cha Ahlulbait (a.s) katika kipindi chote cha mwaka.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: