Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi amesema kuwa, fatwa ya kujilinda na muitikio wa wairaq wa haraka na kujitolea kwao ndio sababu ya kuwashinda magaid wa Daesh.
Ameongea na ugeni wa wanafunzi wa kidini kuhusu umuhimu wa kukumbuka fatwa iliyotolewa na Mheshimiwa Marjaa mkuu Sayyid Sistani iliyolinda taifa la Iraq na raia wake dhidi ya magaidi wa Daesh.
Akasema: “Matukio yaliyoshuhudiwa Iraq na nafasi ya Marjaa Dini mkuu na fatwa tukufu ya kujilinda aliyotoa dhidi ya Daesh, sambamba na muitikio wa haraka ulio patikana ambao hautasahaulika duniani na katika ulimwengu wa askari, hakika raia walikuwa wanajua kuwa Daesh wapo kwenye batili na fatwa ni ya haki, wakaweza kupambanua baina ya mambo hayo mawili bila kusita.
Akaongeza kuwa “Walioitikia wito wa fatwa ya kujilinda walikua na msimamo imara, ushuhuda unaopatika kwa familia zao ni mzuri, baadhi yao walikuwa wanasema tunataka kumliwaza bibi Zaharaa na Ummul-Banina (a.s)”, akasisitiza kuwa “Hakika waliweza kutambua haki na kuinusuru kutokana na Imani yao kwa Ahlulbait (a.s)”.
Sayyid Swafi akasisitiza kuwa waandishi wa Habari wanatakiwa kuweka umuhimu katika kuandika visa vyao na namna walivyo jitolea, hakika walijitolea kila kitu kwa ajili ya kulinda taifa lao na maeneo matakatifu.
Akabainisha kuwa “Mtu mwenye Dini lazima atakuwa na namna ya kujilinda na fikra potofu zinazoingizwa katika jamii ya kiislamu”, akasema “Mwanaadamu hupitia hatua tofauti katika umri wake hadi kufika katika hatua ya kuweza kupambanua baina ya haki na batili”, akabainisha kuwa “Kuna milengo miwili ya wazi, mlengo usio kubali batili na mlengo usiokubali haki, mlengo usiokubali batili ndio mlengo wa Ahlulbait (a.s) na wanachuoni, na mlengo usiokubali haki hujipambanua kidogo kidogo”.
Akaendelea kusema kuwa “Hakika baadhi ya watu waliokuwa katika kundi la wapinzani wa bwana wa mashahidi (a.s) walikuwa na uwelewa, walijua Imamu Hussein (a.s) yuko kwenye haki, lakini dunia iliwafanya wasimame pamoja na wapinzani wa Imamu, wakakosa vyote dunia na akhera”.
Sayyid akasisitiza walimu kujenga uwelewa sahihi katika jamii na kufundisha misingi sahihi ya uislamu na mwenendo wa Ahlulbait (a.s).