Rais wa kitengo Sayyid Dhargham Raadi amesema “Kulikuwa na mawasiliano kati ya idara ya kuhuisha maadhimisho katika kitengo chetu na kitengo cha Mawakibu na vikundi vya Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu, kuhusu kuwasiri kwa mawakibu za watu wa Karbala, waombolezaji wamepokewa kwenye malango ya mji wa Kadhimiyya kwa kupitia mlango wa Muradi”.
Akaongeza kuwa “Atabatu Abbasiyya imezowea kusaidia Atabatu Kaddimiyya kwenye ziara zinazohudhuriwa na mamilioni ya watu, sambamba na vitengo vingine vilivyoshiriki kutoa huduma”.
Maukibu ya Atabatu Abbasiyya hutoa huduma kwa mazuwaru wakati wa kuomboleza kifo cha Imamu Muhammad Aljawaadi katika mji wa Kadhimiyya kila mwaka, kwa muda wa siku nne.